DONALD TRUMP AHAIDI KUSHUGHULIKIA HATUA YA KOREA KUSINI KUJARIBU KOMBORA LA JANA.
Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis.
Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan.
Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi.
Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba.
Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo.
Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya hivi karibuni.Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo linaweza kufika mahala popote pale duniani
Bwana Mattis amesema kuwa kombora hilo liliruka juu ikilinganishwa na kombo jingine lolote lile hapo awali.
''Korea Kaskazini ilikuwa ikiunda kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine ambalo linaweza kurushwa eneo lolote lile duniani'', aliongezea.