Wednesday, 29 November 2017


DONALD TRUMP AHAIDI KUSHUGHULIKIA HATUA YA KOREA KUSINI KUJARIBU KOMBORA LA JANA. Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis. Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan. Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini. Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi. Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba. Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo. Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya shutuma kutoka kwa jamii ya kimataifa. Baraza kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya hivi karibuni.Waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo linaweza kufika mahala popote pale duniani Bwana Mattis amesema kuwa kombora hilo liliruka juu ikilinganishwa na kombo jingine lolote lile hapo awali. ''Korea Kaskazini ilikuwa ikiunda kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine ambalo linaweza kurushwa eneo lolote lile duniani'', aliongezea.

Wednesday, 8 March 2017

BREKING NEWS NI KWELI KUNA CHETI CHA ZERO KAMA MAKONDA ALIVYOSEMWA, MAGUFULI ATAMKA.


[BREAKING NEWS]::KUHUSU ISHU YA VYETI FEKI RAIS MAGUFULI AMJIA JUU ASKOFU GWAJIMA AMJIBU HAYA KUHUSU VYETI VYA MAKONDA,TAZAMA HAPA LIVE KABISA NIMEKUWEKEA LIVE GWAJIMA TUNA SHUKURU KWA KUTUJUZA KUWA UNA VYETI VYA MAKONDA ,NDUGU GWAJIMA MTUMISHI WA MI UNGU POLE SANA KWA KUTAJWA KATIKA ORODHA YA WATU WANAO HUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA , MIMI KAMA MTANZANIA NINA MACHACHE KWAKO ,1 WE MTUMISHI WA MI UNGU UNAPITIWA SANA KATIKA MAAMUZI YAKO ULISEMA HUTA MSHITAKI MAKONDA NILIFURAHI NIKAJUA KWELI UNA MOYO WA MSAMAHA 2,, UKASIKIKA TENA KWAMBA UTA MRUSHIA MAPEPO WENGI TULIPIGWA NA BUTWAA 3,, UKAJA NA HABARI YA VYETI VYE ZIRO TUKA SHANGAA ,TUKA JIULIZA HUYU MTUMISHI WA MI UNGU KULIKONI ?, GWAJIMA DHAMANA ULIYO NAYO NI KUBWA MNO KIONGOZI WA DINI KUZUSHA JAMBO NI AIBU SANA , NATOA WITO KWA VIJANA WENZANGU MAKONDA HAWEZI KUTOA VYETI HADHARANI KWANI HATA GWAJIMA HAJATOA VYETI HADHARANI NDANI YA ARIDHI YA TANZANIA HAKUNA CHETI CHA ZIRO, NAMSHAURI GWAJIMA KAMA ROHO INA MUUMA AMA ANATAKA KULIPA KISASI UFUNGUWE KESI YA KUVUNJIWA HESHIMA , JAPO NAAPA ASILANI ABADANI HUWEZI FANYA HIVYO UTAKUWA UMEJIMALIZA , WATANZANIA SIYO WAJINGA KIASI HICHO CHA KUAMINI UNA VYETI VYA ZIRO==>>http://b

Friday, 3 March 2017

MAGAZETI YA LEO TAREHE NNE JUMAMOSI HABARI ZA LEMA

"text-align: left;" trbidi="on">

MAMA SALMA ANA HAKI YA KIKATIBA KUTEULIWA MBUNGE KAULI YA ZITTO KABWE


Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa maoni yake kuhusu uteuzi wa mke wa Rais Mstafuu Jakaya Kikwete, Salma Kikwete kuwa Mbunge. Machi Mosi mwaka huu, Salma Kikwete aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilisema kuwa, Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge. Hapa chini ni maoni ya Zitto Kabwe aliyoyatoa kupitia ukurasa wake wa Facebook. Siku nzima ya jaa nilikuwa natakiwa na waandishi wa Habari kutoa maoni yangu kuhusu uteuzi wa Mtanzania mwenzetu, na mke wa Rais aliyepita, Mama Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Niliwaambia sina maoni yeyote. Leo baada ya magazeti kuandika maoni ya watu mbali mbali nimeulizwa tena. Jibu langu, ambalo ninaliweka hapa kwa umma, ni kwamba Mama Salma Kikwete ana haki zote kama Mtanzania mwengine yeyote kuteuliwa ama kuchaguliwa Kwa mujibu wa Katiba yetu. Hivyo uteuzi wake kwa maoni yangu ni kama teuzi nyengine zozote zile. Kuolewa kwake na aliyekuwa Rais hakumwondolei yeye haki zake za kikatiba. Kama mwenyewe ataridhia ninamtakia kila la kheri katika kazi yake mpya. Sababu za kuteuliwa kwake anajizuia aliyemteua na baadhi ya wasomi wabobezi Kama Prof. Kitila Mkumbo wamenukuliwa wakifanya uchambuzi mzuri Kabisa kwenye gazeti la The Citizen la Leo. Kwangu Mimi, kwa maoni yangu, nchi yetu inakabiliwa na mambo makubwa zaidi ya kujadili na kutolea maoni ikiwemo suala la njaa. Serikali kwenye suala hili la njaa imeyumba sana na kwa kiasi flani imewayumbisha pia wananchi wanyonge wanaokabiliwa na tatizo hili, na kwa maoni yangu naamini kabisa Serikali haijatekeleza wajibu inavyostahili. Kama mzalendo kwa taifa langu nachukua wajibu wangu kuonyesha mapungufu hayo ya Serikali pamoja na kutoa njia mbadala. Jana, Serikali kupitia Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kusisitiza kuwa haitatoa chakula cha msaada kwa Watanzania watakaokabiliwa na njaa. Rais alisema “tumezoea kuambiwa maneno matamu matamu kwamba hakuna mtu atakeyekufa kwa njaa. Mimi nawaambia usipolima utakufa na njaa”. Serikali kwa kauli za namna hii inawachanganya watanzania, kwanza ni muhimu sana kujua (na naamini Serikali inajua) kuwa wananchi hawa wamelima, suala la hali ya njaa si kwa sababu ya kutokulima kwao, bali ni kwa sababu kadhaa zilizo nje ya uwezo wao, ikiwemo hali ya hewa yenye mvua chache. Mfano mikoa ya Singida, Shinyanga na Tabora wananchi wetu walilima, lakini mvua hazikunyesha kabisa, mahindi yalikauka na majaruba ya mpunga hayakuwa na maji kabisa kati ya mwezi Desemba na Januari ambacho ndio kipindi cha msimu wa Kilimo kwa mikoa hiyo. Sasa Serikali kupitia Rais inapowaambia wananchi kuwa ‘wasipolima watakufa na njaa’ si sawa, ni kama vile tunaihusianisha njaa na wao kutolima, jambo ambalo si kweli. Rais wetu sio tu ni Amiri Jeshi Mkuu wa Taifa letu (Commander In Chief) bali pia anapaswa kuwa Mfariji Mkuu (Comforter In Chief) kwa watu wetu katika nyakati za majanga kama matetemeko ya ardhi, mafuriko na ukame ambao unasababisha njaa. Kazi kuu ya Serikali yoyote ni ugavi wa matumaini kwa wananchi, na Rais wa nchi anapaswa kuwa Kiongozi wa kugawa matumaini hayo, hatusemi serikali itoe matumaini hewa, lakini pia hatukubali serikali ‘ivunje moyo wananchi’ kwa kuhusisha hali ya ukame na wao kutokulima. Hili si sawa. Januari 31, mwaka Serikali ilitoa tamko juu ya suala la njaa, tamko husika lilitolewa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, kwamba kuna Halmashauri 55 zinazokabiliwa na njaa na kwamba Serikali itapeleka chakula cha bei nafuu ili kuhakikisha kuwa wananchi katika Halmashauri hizo 55 hawafi njaa. Serikali hapa ilichukua jukumu lake la kutoa matumaini kwa wananchi hawa. Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi ni mteule wa Rais, ni sehemu ya Serikali hii, sasa mkuu wa Serikali husika anaposema kuwa ‘watu walime na hakuna chakula cha msaada’ anafuta matumaini haya, na si tu kufuta matumaini kwa wananchi lakini pia anawachanganya wasaidizi wake ambao wanaweza kuogopa kutekeleza msimamo wa Serikali uliotolewa bungeni na Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi wa kupeleka chakula cha msaada katika Halmashauri hizo 55. kuogopa kupeleka chakula maeneo yenye njaa na hivyo kusababisha watanzania kupoteza maisha. Ninarudia kauli yangu kwamba iwapo Mtanzania yeyote atakufa kwa njaa hatutakuwa na budi kumwajibisha Rais kwa kutumia Katiba. Utafiti wa Shirika la TWAWEZA wa mwezi Februari 2017 unaonyesha kuwa Theluthi ya Watanzania ( Watanzania 17 milioni) Hivi sasa wanalala njaa ama kushinda na njaa. Pia nusu ya Watanzania wanakabiliwa na upungufu wa chakula. Hawa wanahitaji matumaini kutoka kwa Serikali na sio taarifa mbili tofauti za Serikali zinazojikanganya. Ni muhimu wananchi waelewe kuwa suala la njaa na ukame si jipya nchini, mwaka 2006 na 2007 nchi ilikumbwa na ukame mkubwa sana na Rais wa wakati huo alitamka kuwa “hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa”. Tuliona Serikali nzima chini ya kiranja wao, Waziri Mkuu ikizunguka nchi nzima kuhakikisha kuwa ‘hakuna Mtanzania anakufa kwa njaa’. Kwanini Serikali ilifanya hivyo mwaka 2006/7? Ni kwa sababu KATIBA inatamka kuwa kila Mtanzania ana haki ya kuishi na ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa haki hii ya kuishi inalindwa. Ndio maana Serikali ilianzisha Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA) kwa lengo la kuhakikisha tuna akiba ya chakula cha kutosha, na kwamba ikitokea kuna majanga ya asili kama ukame basi ‘Mtanzania hafi kwa njaa’. Naiasa Serikali itekeleze wajibu wake huu wa Kikatiba – ihakikishe hakuna mtanzania anayekufa kwa njaa. Kushindwa kufanya hilo ni kushindwa kulinda Katiba.

Sasa nambari moja ya simu kutumika katika mitandao yote Tanzania


Katika kuboresha kiwango cha huduma ya mawasiliano ya simu nchini Tanzania, Mamlaka ya mawasiliano TCRA imeanzisha mfumo wa utumiaji namba moja katika mitandao yote ujulikanao kama mobile number Portability... lakini ujio wa mfumo huo umepokelewaje na walengwa?

NAMSHUKURU SANA MKE WANGU NINGEPATA NAFASI YA KUMUOA NINGEMUOA TENA.KAULI YA LEMA BAADA YA KUTOKA RUMANDE


Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo March 3, 2017 imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambapo Mahakama hiyo ilimtaka Lema asaini bondi ya shilingi milioni 1 na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika ambapo alikidhi vigezo na kuachiwa huru. Baada ya kuachiwa kwa dhamana mbunge Lema ameyazungumza haya.…….>>>“Namshukuru sana mke wangu na kama ningepata fursa ya kumuoa ningemuoa tena yeye, nikisema niongee leo sitaweza nimeandaa waraka kwa ajili ya mheshimiwa Rais na nitautoa hivi karibuni nimeona mateso mengi ya watu”-Mbunge Lema.

Thursday, 2 March 2017

HATIMAYE KENYA KUIPIGA ALSHABABU


Jeshi la Kenya limesema kuwa wameua wapiganaji 57 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab katika mapambano huko kusini mwa Somalia mapema wiki hii. (Jumatano) Waziri wa ulinzi wa Kenya amesema kuwa Vikosi chini ya majeshi ya umoja wa Africa (amisom) vilitumia mashmbulizi ya anga dhidi ya waasi hao karibu na mji wa Afmadow, takribani kilometa 100 kaskazini magharibi mwa Kismayo. Lakini Al-Shabaab walikana juu ya taarifa hiyo ya kuuawa kwa wapiganaji wake.